Go down
avatar
Admin
Admin
Posts : 8
Points : 237
Reputation : 0
Join date : 2019-10-04
Age : 19
Location : Morogoro
https://swahililand.africamotion.net

Njia kumi za kutengeneza pesa mtandaoni Empty Njia kumi za kutengeneza pesa mtandaoni

on Sun Dec 22, 2019 4:29 am
Njia Kumi (10) za uhakika za kuengeneza Pesa Mtandaoni
Najua umeona sehemu nyingi watu wamekuwa wanakuonyesha moja ya njia hizi bila ya kuwa na uhakika na wanachokiandika sasa katika post hii nitakuonyesha njia 10 za uhakika za kutengeneza pesa mtandaoni kwa kutumia simu na kompyuta endapo mtu atajituma bila kuwa na project nyingi katika mitandao na tuanze na njia ya kwanza hadi ya mwisho katika orodha hii 
Anzisha Blog 
Hii ni njia maarufu kwa wengi na unaweza kuona watu hapa Tanzania na afrika mashariki kama millardayo na lemutuz wanavyoingiza kipato kizuri kupitia blogging nah ii haihitaji wewe kuwa na kipato, ni wewe na maandishi na picha zako zenye kuvutia wasomaji ili uwe na uhakika wa kuingiza pesa kupitia mtandao. Angalia mambo matano ya kuzingatia kabla ya kuunda blog. 
Affiliate Marketing.
Hii ni njia ya pili ambapo mwenye tovuti analipwa kwa sababu ya kuwashawishi wasomaji wake kununua bidhaa anazozitangaza kutoka mitandao kama Rakuten,Amazon na Alibaba na mingineyo ,nay eye hulipwa commission pale mtu(mteja) anaponunua bidhaa hizo kutoka kwenye blog au Tovuti yake kwa kila bidhaa atakayouza.Bonyeza hapa kujua affiliate marketing kwa undani.
Uza Bidhaa Mtandaoni.
Achana na kutangaza bidhaa kupitiya kupatana.com,Guliostore ,Jiji Tz,Bongofree namaanisha Tengeneza E-Commerce Site kama kikuu.co.tz na uuze bidhaa kama Electronics,Nguo,Vitabu kama vile Amazon.com na platform nzuri za kumanage E-Commerce site yako ni 
⦁ Shopify
⦁ Woo Commerce
⦁ Big Commerce
⦁ Magento
Tengeneza Youtube Channel kuelimisha au Kuburudisha
Nadhani umeshuhudia watu wengi Tanzania na Africa masharki wamejikita kwenye youtube kuliko sehemu zingine nilizozitaja mfano Millardayo,OphoroTube,Lemutuz wakipoke tuzo zao kutoka youtube
 
Kwa sababu ya kufikisha Subscribers laki moja(100,000) na kujua njia hii kwa undani Zaidi Bonyeza Hapa.
Uza E-Books
eBook ni kitabu cha kidigitali chenye mfumo wa Pdf ambacho huweza kusomwa na kifaa chochote. 
Hii ni njia nyingine kwa wale wanaoandika vitabu na hawana kipato cha kutosha cha kuchapisha .eBook haihitaji kuchapisha ,ni kuandika vizuri kukipangilia na kuweka Amazon kusubiri manunuzi.Mfano mzuri ni Michael Mkwanzania ambaye ana Kitabu chake “Biashara Mtandaoni” ambacho ni Beginer na Advanced Course anachokiuza kupitiamkwanzania.thinkfik.com
 
Kufanya Surveys(Kujibu maswali nk).
Hii ni njia mojawapo ya kupata pesa mtandaoni kwa kujibu maswali na kubonyeza Tovuti na mwishowe kupata coins ambazo utaweza kuzibadilisha na kuwa pesa katika mfumo wa dollars.
Na tovuti hizi ni Get-paid.com,Survey Junkie na Swagbucks .
Tengeneza kozi Mtandaoni.
Hii ni njia nzuri kwa wale wenye ujuzi wa kidigitali kama Adobe Photoshop,Blogging,Online marketing na mtandao kwa ujumla au ujuzi wowote unaoweza kuuonyesha Mtandaoni kupitia Skillshare.com au Tovuti yako mwenyewe kutumia thinkfic.com.
Teneneza Tovuti(website) 
Hii ni njia mojawapo ambayo inaweza kukuingizia pesa endapo utapata wateja wasiopungua watano(5). Unaweza kuanza kwa kuomba tenda ya kuunda Tovuti za Makampuni mbalimbali na blog kwaajili ya media house Mbalimbali Mfano Basil Lyayuka mwenye kampuni ya Idodoe ambayo imetengeneza millardayo.com.
 
Tengeneza Mobile Application.
Hii ni njia inayotumiwa na vijana wengi Tanzania wenye ujuzi wa kutengeneza mobile application kama kampuni ya Dau Technologies LLC iliyotengeneza apps kama SimGazeti,Uwaridi na Hea ambazo zote zinalipiwa na watumiaji ili waweze kupata content.
⦁ Kumanage Social Media za Makampuni.
Hii ni njia ya mwisho katika Orodha hii ambapo makampuni makubwa ya habari na biashara zingine huhitaji watu wenye uwezo wa kumanage account katika mitandao ya kijamii kama Facebook,Twitter ,Instagram na mingineyo.
Twisted Evil Question afro
Attachments
Njia kumi za kutengeneza pesa mtandaoni Attachment
58442914_1033653373502721_4819709319140343808_o.jpg You don't have permission to download attachments.(170 Kb) Downloaded 0 times
Back to top
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum